Kanisa nchini Uingereza lajibu wito kwa Uinlilishaji mpya
Kanisa la Uingereza kujibu wito wa Papa Francisco Kanisa la Uingereza limejibu
wito wa Papa Francisco alio utoa kwa Jumuiya zote zitafute njia za kufanya kwa ajili
uinjilishaji katika nyakati za sasa. Imewezekana kufanikisha ombi la Papa kupitia
mpango wa Parokia ya Mtakatifu Maria Mjini Grimsby Uingereza, ambapo waamini wameongezeka
idadi ya kwenda katika ibada Misa. Katika kufanikisha tukio hili vifaa muhimu
vya unjilishaji vilisambazwa katika Parokia za Uingereza na Wales, kwa ajili ya
maandalizi ya tukio la siku ya umissionari Jumapili 21Septemba ikiwa na kaulimbiu
Uinjilishaji, katika moyo wa familia”. Taarifa kutoka katika “gazeti la Oservatore
Romano” limemkariri Askofu wa Arundel na Brighton Munsinyo Kieran Thomas Conry, ambaye
ndiye mhusika wa kitengo cha uinjilishaji. Wajumbe wa kamati hiyo ya mpango, Paroko
wa Parokia ya Mtakatifu Maria wa Bahari, Padre Clare Ward na padre Joe Wheat na
Ann Casson waliendesha mafunzo muhimu kwa waamini kama njia mpya ya uinjilishaji. Askofu
aliongeza kwamba walikuwa wanafahamu waamini wengi hawaendi katika ibada ya Misa
lakini walitaka kujua sababu zake ni nini,baada ya kukutana nao waligundua kuwa hakuna
sababu maalumu, bali watu wakiacha kwenda kanisani kwa muda inakuwa vigumu kurudi.
Inawaogopesha , na kujisikia aibu ya kuonekana namna gani kanisani, aliongeza Askofu
Conry Katika mpango wao wenye jina “kuvuka kizingiti” waliamua kuwapa matumaini
wana parokia ili kuweza kuwafikia waatoliki ambao wako mbali na kanisa ili wapate
kurudi , kwani kanisa linalowapokea na linawahtaji. Haijalishi wingi wao wa kurudi
kanisani, la muhimu wao watambue kwamba kanisa linawasubiri daima. Aliongeza Askofu. Naye
mkurugenzi aliyetengeneza mpango huo wa iunjilishaji wa Baraza la Maaskofu Uingereza
wa parokia tano za Lincolnshire na kanisa kuu la Nottinghan alisema , kile tunachojali
ni ule uhusiano wa moja kwa moja na wakristo, wakristo wanaoudhuria kanisa wanapaswa
wajisike vizuri, bila kuyumba , katika mioyo yao, ili kuweza kuwakaribia hata wengine
walio mbali na kanisa. Alitoa mfano jinsi walivyofanya kuwavutia warudi kanisania
akisema kuwa ,kitu kilichofanyika ni njia ndogo na hasa ile ya matukio yao ya kila
siku kwa kupitia utamaduni wa siku ya Mtakatifu Teresa wa mtoto Yesu. Vilevile Kanisa
kuu la Nottingham liliamua kufungua milango kila siku jioni kuabudu Ekaristi Takatifu. Aliendelea
kwa njia hizi kumefanya kuongezeka kwa waamini katika parokia kufikia asilimia miamoja.
Kwa upande wa kitengo cha unjilishi ni mwafaka na muhimu kujifunza njia zaidi za kumfikia
aliyepoteza njia yake ya imani. Pamoja na mafaniko hayo kwenye mpango huo wa uinjilishaji
katika Parokia hizi tano Paund 600 za Uingereza zilitolewa na Baraza la maaskofu katoliki
la Uingereza na Galles . Idadi ya waamini wengi walioanza kurudi katika kanisa na
hasa kwenye mkesha wa pasaka ni waamini kutoka Parokia ya Mtakatifu Maria juu ya
Bahari Grimsby eneo ambalo linahesabika kuwa la nne kwenye umasikini nchini Uingereza.
Vilevile Padre Joe Wheat alisema kwamba kuongezeka kwa watu hao kulitokana na kuwakaribisha
wazazi na watoto wao wadogo katika shughuli mbalimbali za kuchora na kutengeneza sanaaa
kwa kipindi cha pasaka, ambapo pia walipaka rangi mayai kama utamaduni wa sehemu nyingi
za Ulaya. Aliendelea ya kwamba; walikuwa wakisubiri watu kama ishirini tu lakini
, na matokeo yake wakafika watu 80, na kipindi cha sikuku ya kuzaliwa kwa Bwana,waliweza
kuweka matangazo wa kuwajulisha juu ya misa itakayofanyika usiku kwenye mwanga wa
mshumaa jambo ambalo liliwavutia wengi hadi watu miamoja waliweze kudhuria misa takatifu
ya Noel. Njia ya kuwagawia karatasi mlangoni kabla ya kuanza misa ili wafutile
nyinmbo na kujibu sehemu zote za sala zimewezakusaidia waaamini, vilevile maandalizi
ya hija na kufanya njia ya msalaba wakzingukia mitaa na miji ni mpango ulio wasaidia
waamini kujitokeza na kushiriki , ni ishara ya kuonyesha uwep wa wakristo aliongeza. Kwa
hayo yote Askofu Conry alimazia akikumbusha kwamba Kazi inayofanyika siyo ile ya kutaka
kuwaeleta wote kanisani bali kwa nguvu, shughuli hiyo kichungaji ni kwamba waamini
wajisikie wanathamaniwa na Kanisa , na Kanisa linawasubiri kushiriki katika maisha
yao kila na zawadi msingi za maisha.