Uwepo wa Wakristo Nchi Takatifu, ni rasilimali watu
Patriaki Fouad Twal, Upatriaki wa Yerusalem ya Mashariki, amesema uwepo wa wahamiaji
Wakristo katika Nchi Takatifu kwa sababu mbalimbali kama wafanyakazi na wafanya biashara
na wachuuzi, ni sehemu ya utajiri wa kanisa na zawadi katika eneo hilo, kwa kuwa watu
hao pia hushiriki ktika shughuli nyingine za kijamii zikiwezo za kisiasa. Patriaki
wa Yerusalemu ya Mashariki Fouad Twal, ameonyesha kutambua mchango msingi wa jamii
ya Wakristo wahamiaji ambao huendelea kuwakilisha kweli msingi na muhimu katika miji
mingi ya Israel, kuanzia mjini wa Tel Aviv.
Patriaki Twal, alieleza haya mwishoni
mwa wiki iliyopita wakati akifanya ziara ya kichungaji kwa Jamii ya Kikristo ya eneo
la Jaffa , ambako alitaja uwepo wa Wakristo hao ni ishara muhimu ya heshima na shukrani
kama ilivyoripotiwa na vyanzo rasmi ya Upatriaki. Patriaki Twal, akikutana na Wakristo
wa eneo hilo, aliivutiwa na uvumilivu wa Wakristo jamii ya Hindi na Ufilipino, ambao
ni jumuiya ya kikristo ya wahamiaji wanaoishi katika hofu ya kuwa kafara wa kufukuzwa
katika maeneo waliyokimbilia na mahali wanapo ishi kwa pamoja. Akiwa katika eneo hilo
la Jaffa, Patriaki aliwasisitiza umuhimu wa kujumuika pamoja ktiaka Ibada za Jumapili,
kugundua manufaa ya ushirika miongoni mwa jamii mbalimbali kama chanzo cha utajiri
wa kuheshimiana, na kutambua kwamba wao ni Kanisa moja, Kanisa la Mungu.