2014-09-19 08:42:26

Baada ya mafuriko Kashmir imeporomoshwa “ground zero”- Askofu


Shirika la habari la Fides limemnukuu Askofu Peter Celestine , akieleza kwamba, "Hali ya Jammu na Kashmir baada ya maafa mabaya ya mafuriko ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya eneo hilo, maisha ya watu yamerudishwa nyuma katika hatua ya mwanzo “ground zero”, yakiwa yamepinduliwa kabisa na kuingizwa katika ufukara wa kupindukia. Wakristo ni kati ya waliokumbwa vibaya na mafuriko hayo.

Askofu Peter Celestine, wa Jimbo Katoliki la Jammu-Srinagar, ametoa ombi kwa Jumuiya ya kimataifa kutenda kidharura kwa ajili ya upatikanaji wa misaada ya misaada ya kibinadamu. Amesema, maelfu ya watu maisha yao yako katika hatari za kuangmia kutokana na ukosefu wa mahitaji msingi ya kijikimu. Na kwamba, Kanisa Katoliki, linajaribu kila uwezekano wa kujibu hali hii mbovu, lakini ni wazi limezidiwa nguvu. Wanahitaji msaada wa kidharura wa chakula na maji ya kunywa, makazi ya muda, dawa kwa watu walioathirika. Karibia asilimia 90 ya walioathirika ni familia za Kikristo. Licha ya watu hao pia mali za taasisi nyingi za Kanisa zimeharibiwa na hivyo hasara ni kubwa.

Eneo la Malakar Sudan Kusini limeathirika vibaya na vita-Shahidi aeleza
Sista Helen Balatti, wa eneo la Malakar Sudan Kusini, ametaarifu kwamba, bado kuna hali ya wasiwasi na ukosefu mkubwa wa utulivu, kwa idadi kubwa ya watu wanaoishi katika mji Mkuu wa Malakar wa Mkoa wa Upper Nile, ambako kumekuwa kama kituo cha mapigano kati ya Maaskari wa serikali ya Sudan Kusini na waasi wanaomuunga mkono aliyekuwa Makamu wa Rais, Riek Machar.

Sista Helena, Mkomboni, ameshuhudia hilo wakati akiwasiliana na shirika la habari la Fides hivi karibuni, kwamba Mji huo ambao kabla ya machafuko ulikuwa na wakazi karibia 250,000,kwa sasa umebaki kuwa makao ya wanajeshi. Na kwamba, pamoja na mikataba ya kusitisha mapigano, hali bado ni teke sana katika eneo hilo. Hivyo pia hata vyombo vya mawasiliano vimaeathirika, kama ilivyo jionyesha wakati wa kufungwa kwa Redio Bakhita ya Jimbo Kuu Katoliki la Juba, ambayo imefunguliwa tena wiki hii, baada ya kufungwa kwa karibia mwenzi mzima.
Maelezo ya Sista Helena yalirejea hasa tukio la mwisho la mapigano ya kivita yaliyotokea karibu na mji wa Malakar Agosti 21, majira ya asubuhi ambako walisikia sauti ya mabomu, na kama ilivyokuwa kwa wakazi wengine wa eneo hilo,pia wao Masista waliondoka katika nyumba yao ya kitawa na kutafuta sehemu nyingine ya kujihifadhi kwa usalama wao. Na kwamba kwa sasa wamepata uzoefu wa kutosha jinsi ya kukabiliana na ukatili wa wanamgambo wa upinzani. Katika kipindi cha miezi sita iliyopita, Malakar imeshuhudia mashambulizi kama sita ndani ya miezi michache

Sista, anaeleza uharibifu unaoendelea katika mji huo wa Malakar ambao ni mji wa pili kwa ukubwa Sudan Kusini, kwamba, kwa sasa hakuna tena nyumba za tofali, ila vimebaki vibanda.
Cartas Internationalis yakamilisha mkutano wake.
Shirika la Kimataifa la Caritas Internationalis, Alhamisi lilikamilisha mkutano wake juu ya uratibu wa misaada inayotolewa wakati huu wa mgogoro katika Mashariki ya Kati.
Viongozi Caritas wa Mashariki ya Kati, hasa walilenga juu ya utoaji wa msaada wa kuonekana kwa wagonjwa mahututi, na wale wanaosumbuliwa na kiwewe cha ukatili wa vita. Mkutano huu wa siku tatu, ulifanyika mjini tarehe 15-17 Septemba na wajumbe walijadili hasa uratibu kikanda na kimataifa kukabiliana na mgogoro wa katika Mashariki ya Kati.

Katibu Mkuu wa Caritas Internationalis, Michel Roy amesema, walilenga hasa katiak wajibu wao wa kuipa tumaini jamii ya Mashariki ya Kati, na utoaji wa misaada kwa matawi ya Caritas ya Mashirika ya Kati, katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa, bila kujali tofauti za kidini , bali katika kuhimiza utu na haki za baindamu zinaheshimiwa, ili kwamba, kila mtu awe na uhuru wa kuishi kwa amani na jirani zao.
Waziri wa zamani wa serikali Damianos Kattar kutoka Lebanon alieleza kuwa mahitaji ni makubwa sana, kiasi kwamba peke yao hawaezi kitu. Alifafaanua kwamba , nchini Syria pekee, leo hii inahitaji kiasi cha dola bilioni $ 100 kukidhi mahitaji msingi. Na itachukua miaka kati ya 15-25 ujenzi kuijenga tena nchi baada ya vita hivi. Wakati huohuo, watu wenye msimamo mkali Iraq na Syria wanaendelea kueneza unyama huu wa kimbali na utakaso wa kidini katika maeneo wanayo yadhibiti.. Na hali ya Wapalestina ni kama wanaishi katika gareza wazi,wakinyimwa haki ya utu na hadhi na ardhi yao.
Mkutano huu ulihudhuriwa na Askofu Shlemon Warduni, Rais wa Caritas Iraq, na Padre Raed Abusahliah, Askofu Antoine Audo, Rais wa Caritas na Wawakilishi kutoka Syria na katika Jordan, Lebanon na Uturuki.

Wakristo katika Nchi Takatifu wanaishi chini ya uvuli wa Msalaba wa Kristo, alama ya mateso ya hali ya juu Mashariki ya Kati, alisema Fr Raed Abusahliah, ambaye aliendelea kusema Wakristo wazawa wa eneo hilo, kuondolewa makwao, itakuwa janga kwa dini zote katika kanda hiyo na dunia kwa ujumla.
Mateso ya watu Wakristo wa Yazidis, inakuwa ni mfano halisi wa mateso na wasiwasi, unoawapata waamini wa dini zingine ambao ni wachache katika mikoa mingine kama Palestina na ukanda wa Gaza.

Ebola yaweza kudidimiza uchumi wa Afrika Magharibi
Kuzuka Ebola kunaweza kuathiri uchumi wa nchi za Afrika Magharibi hasa Guinea, Liberia na Sierra Leone, ambazo zimeshambuliwa vibaya na virusi vya ebola, Benki ya dunia imesema.

Taarifa ya Benki hiyo inasema , athari za virusi vya ebola kiuchumi, viko katika mwelekeo wa kuongezeka zaidi katika mataifa hayo ambayo tayari yako katika myumbo tete wa kiuchumi, ambako mpaka sasa virus vya ebola vimekwisha ua watu 2461 Afrika Magharibi.

Rais wa Marekani Barack Obama hivi karibuni alikuita kuzuka vya virus vya ebola kuwa "tishio kwa usalama wa kimataifa," na alitangaza Marekani ina wajibu m kubwa katika kupambana na virusi vya ebola kama ilivyokuwa kupambana na ukimwi. Hatua zinazo chukuliwa na Marekani, pamoja na kupeleka askari wake katika mikoa iliyoatharika kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vituo vya afya zaidi vitakavyoshughulika na huduma mpya ya afya.

Alhamis hii Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilikuwa na kikao cha dharura kujadili janga hili. Ilitazamiwa mkutano kukamilika na azimio linalo dai jumuiya ya kimataifa iingilie kwa nguvu zaidi, tatizo hili, na kuzitaka nchi wanachama kupeleka msaada wa madaktari na kufungua vituo zaidi vya kukabiliana na virusi. Pia azimio linatazamiwa kuzitaka nchi kuondoa vikwazo vya kusafiri kutoka na kuingia yenye kwua na wagonjwa wa ebola, kwa maelezo ya Viongozi wa Umoja wa Mataifa kwamba , hakuna sababu za kufanya hivyo kwa nyakati hizi.
Uchambuzi wa Benki Kuu unaonyesha kwamba, uchumi wa nchi zilizoathirika na virus vya ebola utadodoka kwa mabilioni ya dola ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao wa fedha. Na kamba mpaka sasa tabiri zinaonyesha kwamba, uchumi utapungu a kwa asilimia 2.3 Guinea na Sierra Leone utashuka kwa aslimilia 8.9.
Jengo la Joshua wengi wa waliofariki ni Wasauthi
Kwa mujibu wa takwimu za Jumatano , wengi wa waliofariki katika jengo la Joshua lililo poromoka Ijumaa iliyopita, ni kutoka Afrika Kusini. Inatajwa kati ya maiti zilizopatikana kuna miili 67 ya Wasauthi. Jengo lililokuwa likitumika kama Hosteli, ni mali ya mhubiri Maarufu wa Nigeria , Mwinjilisti Joshua, la nje kidogo ya mji wa Lagos, liliporomoka wiki iliyopita.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameiita ajali hii kuwa mbaya katika historia ya maafa kwa Wasauthi hivi karibuni Viongozi wa Nigeria, wanatajwa kuwa wazito kutoa habari za kuaminika juu ya waliofariki katika ajali hii.
Na katika ujumbe wa rambirambi iliyotolewa na Maaskofu Katoliki wa Afrika Kusini , Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano katika Baraza la Maaskofu, Br S'milo Mngadi, amesema, Maaskofu wameonyesha kusikitishwa na ajali hii. Na wanaziombea roho za marehemu zipate kupumzika mahali pa amani kwa Mungu, familia zao ziweze kufarijika katika ufufuko wa Bwana, na majeruhi wapate kurejea afya njema.

Pamoja na waliofariki watu wengine zaidi ya 130 wamebaki majeruhi.tu wengine ni alisema kuwa kujeruhiwa. Hosteli alikuwa mwenyeji wa Afrika Kusini. TB Joshua ni mkubwa sana maarufu tele-mhubiri katika Afrika.







All the contents on this site are copyrighted ©.