2014-09-17 16:07:42

Katekesi ya Papa Francisco:Katoliki maana yake ulimwengu mzima


Katika mwendelezo wa katekesi juu ya Kanisa, Jumatano papa Francisco emendelea na sehemu ya kanuni ya imani, kwamba tunapotamka nasadiki kanisa katoliki,ina maana gani ya maneno haya mawili na pia yana maana gani katika Jumuiya ya wakristo na watu wote?
Papa alitoa jibu kwamba katoliki maana yake ni ulimwengu mzima.

Aliendelea kwamba jibu kamili lilitolewa na mmoja wa baba wa kanisa katika karne za kwanza, Mtakatifu Cirillo wa Yerusalem, ya kwamba : Kanisa Katoliki bila wasiwasi maana yake ni ulimwengu mzima, kwasababu kanisa limetawanyika mahali popote duniani.Pamoja na hayo kanisa linafundìsha ukweli ambao watu wote wanapaswa kuufikia, yaani mambo yote yanayotazama mbingu na kidunia yanayoelezwa katika Kateksimu ya Kanisa Katoliki § XVIII,23, ni ishara madhubiti ya kanisa katoliki ambayo inaongelewa katika lugha zote za dunia.

Hii ndiyo matokea ya siku ya Pentekoste(cfr At 2,1-13) Ni Roho Mtakatifu ambaye amefanya kazi hii kiasi cha mitume na kanisa zima kusikika hadi miisho ya dunia,ni habari njema ya uokovu na upendo wa Mungu. Kanisa lilizaliwa kwa namna hiyo ya ukatoliki, maana yake ni ” ulinganifu wa sauti nyingi” kwa pamoja kwani haiwezekani iIkawa katolika iwapo haliendelezi, uinjilishaji na kukutana na wote.

Kila lugna inasoma Neno la Mungu, na watu wote wanasoma Injili katika lugha zao. Ni vizuri kurudia maneno hayo ya kwamba, daima ni vizuri kutembea na injili ndogo mfukoni, katika mkoba, ili siku isipite bila kusoma mistari ya Injili . Ni vizuri kufanya hivyo alisisitiza Papa

Injili imeenea kwa lugha zote za Kanisa kwa kuwa ni Neno la Yesu Kristo Mkombozi wa ulimwengu mzima. Na kwa hiyvo wanasema kanisa ni katoliki kwa sababu ni la ulimwengu mzima.

Iwapo kanisa limeaziliwa katoliki , ina maana limezaliwa ili lipate kutoka, na ndiyo maana ukazliwa umisionari. Alitoa mfano “ iwapo mitume wangebaki katika chumba cha Karamu ya Mwisho ya Bwana, bila kutoka nje na kupeleka injili, Kanisa lingebaki na watu wa palepale , mji ule wenye jengo ambamo mna chumba cha karamu ya Mwisho. Lakini wote walitoka kwenda ulimwenguni , siku ambayo lilizaliwa kanisa baada ya kushuka kwa Roho Mtakatifu.

Kwa hiyo Kanisa lilizaliwa kwa ajili ya kutoka nje, maana yake linakuwa la kitume na ndiyo maana tunawaita mitume , kwa maana mtume ni yule anayepeleka habari njema ya ufufuko wa Yesu.

Vilevile neno hili linatukumbusha ya kwamba kanisa limesimikwa juu ya mitume na linaendelea nao, ni mitume waliokwenda kuanzisha makanisa mengine , walifanya madaraja wa maaskofu na kuendelea namna hiyo katika dunia. Leo hii bado kuna mwendelezo wa vikundi vya mitume waliopokea Roho Mtakatifu na pia wao wanatoka kwenda kuhubiri.Wanatumwa kwenda kupeleka habari ya Injili wakisindikizwa na ishara za wema na nguvu za Mungu.

Hii yote inatokana na tukio la Pentekoste, ni nguvu ya Roho Mtakatifu ya kudumu na kushinda vishawishi ambavyo vinaleta ubinafsi wa kujifungia wao kwa wao, wale wachache wanaojifikiria kwamba ni wateule, na kujifikiria kwamba ni zawadi na baraka kutoka kwa Mungu. Iwapo kikundi kimojawapo cha kikristo kinafanya hivyo, cha kujifikiria kimeteuliwa, basi kimekufa. Kwanza kimekufa kiroho, baadaye kitakufa kimwili, kwasababu hawana maisha, hawana uwezo wa kutengeza mahusiano mapya na watu wengine: Hawa siyo mitume.

Ni Roho Mtakatifu anayefanya kwenda kukutana na ndugu wengine, hata wale walioko mbali kwa kila hali, hili waweze kushirikishana tunu msingi za upendo , amani ambayo Bwana mfufuka aliziacha kama zawadi.
Matokeo yake ni nini kati yetu na katika jumuiya zetu, aauliza Papa? Ni sehemu ya kanisa ambayo ndiyo katoliki?
Maana yake ni kuchukulia kundani Wokovu wa mwanadamu, bila kujisikia tofauti au mgeni katika matatizo mengi ya ndugu zetu, bali kuwa wakarimu, kujenga mshikamano nao , vile vile kuwa na hisia za ukamilifu , ulinganifu na maelewano katika maisha ya kikristo na daima kukataa nafasi za ubaguzi zinazatufanya kujifungia wenyewe kwa wenyewe.









All the contents on this site are copyrighted ©.