(Vatican Radio) Mkutano wa sita wa Baraza la Makardinali 9 na Papa Francisco, ulianza
Jumatatu asubuhi katika Jengo la Mtakatifu Marta ndani ya Vatican, na unaendelea hadi
Jumatano 17 Septemba 2014. Baraza la Makardinali 9, ambalo pia linajulikana kama
Baraza la wajumbe tisa, wajumbe wake waliteuliwa na Papa Francisco 13 April 2013 ikiwa
umepita mwezi mmoja tangu alipochaguliwa kuwa Papa. Na 28 Septemba 2013, aliwathibitisha
katika jukumu la kuwa washauri wa Papa, kwa ajili ya utawala wa Kanisa zima la ulimwengu
na katika masuala yanayohitaji uandaaji wa mpango kwa ajili ya marekebisho ya Katiba
ya kitume ya "Mchungaji Mwema”, kwa Idara za Curia ya Roma.
Tangu kutajwa
Baraza mwaka jana lilifanya vikao vyake viwili Oktoba 1-3, 03-05 Desemba, 2013. Kwa
mwaka huu limefanya vikao vinne , Februari, April , Julai , na Septemba Makardinali
Wajumbe wa Baraza ni Kardinali , Rais wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Jiji la Vatican
, Kardinali , Askofu Mkuu Mstaafu wa Santigo de Chile, Kardinali , AskofuMkuu wa
Bombay. Kardinali , Askofu Mkuu wa Munich. Kardinali , Askofu Mkuu wa Kinshasa. Kardinali
OFM Cap, Askofu Mkuu wa Boston, Kardinali , Mkuu wa Kardinali SDB, Arskofu Mkuu
wa Tegucigalpa, Kardinali , Katibu wa Jimbo la Papa na Vatican. Mratibu wa Baraza
hili ni Kardinali Rodríguez Maradiaga na Katibu wa Baraza ni Askofu , Askofu wa
Albano.