2014-09-15 15:53:36

Mahubiri ya Papa ndani ya Kanisa dogo la Mtakatifu Marta


Mama Kanisa Jumatatu hii ameadhimisha kumbukumbu ya Mama Maria wa Huzuni. Baba Mtakatifu Francisko, akitoa tafakari kwa ajili ya adhimisho hili amesema, ni vigumu kwa Kanisa kusonga mbele bila Bikira Maria, aliyeteseka pamoja na mzao wake wa kwanza Yesu. Na ndivyo ilivyo kwa Wakristo, bila Kanisa hatuwezi kusonga mbele. Papa alieleza wakati akiongoza Ibada ya Misa mapema asubuhi Jumatatu hii , katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta mjini Vatican kwa ajili ya Ibada kwa Mama yetu wa Huzuni.

Papa Francisko , alitafakari masomo ya siku, akisema, baada ya Siku Kuu ya Kutukuka kwa Msalaba, sasa tunarejeshwa katika kumwona Mama mpole na mnyenyekevu Maria. Alirejea somo la Waraka kwa Waebrania,ambamo Mtume Paulo anasisitiza maneno matatu ya nguvu tunayoweza kujifunza kutoka kwa Yesu, kuwa ni kujifunza, kutiii na kuteseka. kwamba Yesu alikuwa kinyume na baba yetu Adam, ambaye hakutaka kujifunza kile Bwana achomwamuru, hakutaka kuteseka, wala kutii. Lakini Yesu, ingawa alikuwa Mungu, alikubali kujifunza, kutii na kuteseka, alijinyenyekeza akawa mtumishi wa wote. Na huu ndiyo utukufu wenyewe wa Msalaba wa Yesu.

"Yesu alikuja ulimwenguni, kujifunza jinsi ya kuwa binadamu, ili aweze kutembea pamoja na watu. Alikuja ulimwenguni kwa kutii, na alitii. Na utii huu amejifunza kutokana na mateso. Katika utiii huu wa kuikana nafsi yake mwenyewe, kufedheheshwa, Yesu anakuwa tumaini kwa wafuasi wake. Na watu wa Mungu sasa wanatembea kwa uhakika na matumaini. Na ndivyo kwa Mama Bikira Maria, Eva Mpya, kama Paulo mwenyewe alivyoandika, Yesu anawataka wafuasi wake,kujifunza , kuteseka na kutii.
Papa aliendelea kusema, njili ya Siku inatuonyesha Mama Maria,akiwa chini ya mguu wa Msalaba. Yesu anamwambia Yohane, "Tazama mama yako". Kwa maeneno hayo, Mama Maria anakuwa ni Mama wa wafuasi wote wa Yesu. Hakika Maria ni Mama Yetu.

Papa amesema hili ndilo tumaini la Wakaristo kwamba si yatima, maana wanaye Mama anayewajali, Mama Maria mpakwa mafuta. Na pia Kanisa ni Mama yetu mpakwa mafuta, anayetembea katika njia hiyohiyo ya Yesu na Maria , njia ya utii , njia ya mateso, daima likiwa tayari kujifunza namna yakutembea katika njia ya Bwana.Na kwamba Mama hawa wawili – Maria na Kanisa – hubeba mbele matumaini ya Wakristo. Wakristo wako ndani ya tumbo la mzao wa kwanza wa Maria. Na hivyo bila Maria Kanisa haliwezi kuwepo na bila Kanisa hatuwezi kusonga mbele.







All the contents on this site are copyrighted ©.