Hivi karibu ShirIka la mpango wa Chakula , ( WFP) na Bodi ya Kimataifa ya Michezo
ya Raga ulizindua mpango maalumu ya ukusanyaji wa fedha na kukuza uelewa kama sehemu
ya kupambana na njaa wakati wa kombe la dunia la michezo ambao utafanyika Uingiereza
mwaka 2015. Lengo la mpango huo ni kuhakikisha kwamba kabla ya kufanyika kwa michuano
kufikia mshindi wa tatu maarufu kwa ukubwa ulimwenguni ambayo itaanza September 18
mwakani kesho, kuwepo kwa juhudi za kuchangisha fedha katika mradi uitwao Million
Meal Challenge ya kuwasaidia wanafunzi walioko nchi zinazoendelea kupata chakula. Ushirikiano
wa Kombe la Dunia la Raga ya Kupamba na njaa umefanikiwa katika kuongeza uelewa sawa
na kusaidia kazi ya shirika la mpango wa chakula (WFP) katika kuwalisha watu walio
na njaa duniani. Michuano hiyo itakayofanyika nchini Uingereza inakisiwa kuwa
mikubwa zaidi kuwahi kufanyika, na mashabiki wanazidi kuchangia katika Million Meal
Challenge. Kufikia sasa zaidi ya Dola $ 21,000 zimechangishwa kama kupitia katika
mchango wa hiari, kupitia mauzo ya tiketi, kupitia mtandao nchini Uingerea, huku
mauzo ya tiketi kwa mashabiki wa kimataifa yakizinduliwa September 12.
MKUTANO
WA WADAU KATIKA SEKTA YA MIFUGO MWANZA -TANZANIA Wizara ya Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi, ulifanya mkutano mkoani Mwanza nchini Tanzania wa siku tatu wiki
iyopita kwa ajili ya sekta ya mifugo kwa mikoa yenye mifugo mingi na kuwashirikisha
wakuu wa mikoa , wilaya na makatibu tawala. Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika ufunguzi
wa mkutano huo aliwataka wafugaji nchini kufuga kisasa ili kuwavutia wawekezaji kibihashara
na kuongeza kipato kwaajili ya kuondokana na umasikini.. Akivutia umuhimu wa mifugo
alisema "Nyie wadau zaidi ya 400 wa mifugo mliopo hapa, jaribu kubadilika katika suala
la ufugaji, fugeni kisasa ili muone ndege kutoka Ulaya zinafuata minofu ya nyama kama
zilivyokuwa zikifuata minofu ya samaki," Waziri Mkuu alisema endapo wafugaji watajitambua,
kufanya ufugaji wa kibiashara anaamini sekta ya mifugo itakuwa na mchango mkubwa katika
kukuza uchumi wa taifa. Aidha alishangazwa na kitendo cha mkulima anayelima mazao
kwa shida kuishi bora kuliko mfugaji anayepata mifugo mingi bila kutumia mtaji mkubwa. Waziri
Pinda alizungumzia njia mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kwa
wafugaji ikiwa ni pamoja na kupunguza migogoro ya ardhi isiyokuwa ya lazima, kuimarisha
miundombinu katika ufugaji ikiwa ni pamoja na kuboresha malambo, malisho ili kuifanya
mifugo isitange tange kutafuta sehemu ya malisho. Pia aliwataka watendaji mbalimbali
kujitoa nje na kufanya kazi kwa kuanzia ngazi ya chini, kati hadi juu ili kujua matatizo
ya wafugaji hatua aliyosema kwa sasa iko katika hali nzuri. Kuhusu changamoto zinazokabili
sekta hii ya ufugaji Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kamani alisema
wafugaji wa asili wanachangamoto nyingi ambazo kunatakiwa nguvu ya pamoja katika kuzikabili,
na changamoto hizo ni pamoja zana duni za malisho ambapo tatizo hilo linaendelea
kuongezeka hasa kwa wakati wa kiangazi ambapo malisho hupungua kwa kiasi kikubwa. Hata
hivyo, alisema serikali inaokoa zaidi ya Sh.trilioni 20 kutokana na kutumia chakula
kinachotokana na mifugo na kwamba ingekuwa kuagiza nje ingekuwa na ugumu. Aliongeza
jumla ya kaya 1,745 zinajishughulisha na mifugo ambazo ni sawa na asilima 35 ya kaya
4,901 zinazojishughulisha na kilimo na mifugo. Kuhusiana na migogoro ya ardhi
Waziri wa Ardhi Prof. Anna Tibaijuka alisema kuwa matatizo mengi ya ardhi yanatokana
na kuhamishwa kwa mifugo inayosababisha migogoro mikubwa kati ya wakulima na wafugaji.
EBOLA
KUJADILIWA NA WATAALAMU 200 USWIZI Takribani wataalamu 200 wa Ebola wamekutana
huko Uswizi kuzungumzia uwezekano wa tiba na chanjo kwa ugonjwa huo, huku idadi ya
kesi ikiendelea kuongezeka katika mataifa ya Afrika magharibi. Shirika la afya
duniani-WHO linasema mkutano huo wa siku mbili huko Geneva ilikuwa ni wa kutathmini
maendeleo ya karibuni juu ya uwezekano wa matibabu kwa Ebola na kutaja hatua muhimu
sana ambazo zinahitajika kuchukuliwa. Hakuna matibabu au chanjo kwa ugonjwa huu
unaosababisha kifo, japokuwa dawa ya majaribio ya Zmapp, iliyotengenezwa na kampuni
moja ya Marekani imetolewa kwa idadi ndogo ya wagonjwa, baadhi ya wagonjwa hao wamepona. Mkurugenzi
mkuu wa WHO, Margaret Chan alisema jumatano iliyopita kwamba mlipuko wa ugonjwa wa
Ebola katika mataifa ya Afrika magharibi hivi sasa umeuwa zaidi ya watu 1,900 na umewaambukiza
watu wasiopungua 3,500, wengi katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Wakati
huo huoi Nchi ya Sierra Leone ambayo inaongoza kwa ugonjwa huo na Pia Liberia imetoa
tamko kwamba italazimaka watu wake kubaki nyumbani kwa siku nne kuanzia tarehe 18-21Sept
kwaajili ya kugaguliwa na chombo maalumu, kwaajili ya kuzuia maambukizi ya virusi
hivyo. Ni uamuzi ulitolewa na wahudumu wa afya kwaajili ya kuchunguza na kuwatambua
wale ambao wana ugonjwa huo , wasiendelee kusambaza zaidi. Hayo yalielezwa na Bwa
Ibrahimu Ben Kargbo ,mwenyekiti mshauri wa madaktari ya wasio na mipaka nchini Sierra
leone. Bwana alisema hili kupambana na virusi hivyo ni lazima kukabiliana na jambo
hili mara moja; Japo itakuwa ni kazi ngumu kwa wahudumu wa wafya kubaihinisha watu
wenye maambukizi hayo kwa kutumia chombo cha ukaguzi wakibisha hodi nyumba kwanyumba. Pamoja
na hayo alisema kwamba nchini Sierra leon, kunu uhaba mkubwa wa nafas iza wagonjwa
mahosptalini. Ni Zaidi ya wahudumu wa afya 21,000 watakaozungukia nyumba kwa nyumba,
kwa kufuatia hata maelelezo na makubaliano ya mkutano Mkuu wa Afya duniani wa wataaalumu
200 walikutana huko uswizi.