Mkutano wa mwaka wa majadiliano kati ya tamaduni: dunia mashakani
Mwingiliano wa tamaduni na dini katika majadiliano, ni mandhari ya mkutano wa Saba
juu ya Mazungumzano Kati ya Dini, ambao huandaliwa na Baraza la Ulaya kila mwaka.
Kwa mwaka huu mkutano huo umefanyika kwa siku mbili tarehe 1-2 Septemba Mjini Baku,
Azerbaijan. Tukio limewakusanya pamoja, wawakilishi kutoka ndini mbalimbali Wakristo,
Waislamu, Wayahudi, Wabuddhist na hata kutoka makundi yasiyo amani Mungu. Kwa Kanisa
Katoliki, Mjumbe wake ni Pafre Jean-Marie Laurent Mazas kutoka Baraza la Kipapa kwa
ajili ya Utamaduni. Padre Jean Marie Laurent Mazas, akihojiwa na Redio Vatican,
ameeleza lengo la mkutano huo kwamba zaidi ni kuangalia mwelekeo wa kidini katika
mazungumzano ya tamaduni. Na ni dhahiri kwamba, hali ya sasa dunia ni ya wasiwasi
sana, kama Papa Francisco alivyokwisha sema, tuko katika Vita Kuu ya Dunia ya Tatu.
Na hivyo ni muhimu kuwa na mkutano kama huu, si tu kati ya viongozi wa dini, lakini
pia kati ya wenye mamlaka katika Baraza la Umoja wa Ulaya.
Kwa nia hiyo madhumuni
ya Kanisa katika mkutano huu, ni kuongeza kilio cha muumini kwa Mungu, ili kwamba
watu wote wapate zawadi ya amani. Madhehebu yote ya Kikristo, huhubiri maudhui hayo,
na huelimisha kwamba amani ni upendo. Na jambo ambalo daima au kama ni wimbo wao
kwa wote wanaohusika na maamuzi yanayogusa maisha ya jamii ni kwamba mazungumzo kati
ya dini, ni mazungumzo kati ya jamii kwa ajili ya kufanikisha maisha yenye mwingiliano
wa tamaduni bila kuathiri dini wala utamaduni wa mwingine. Na pia ni kushirikishana
mawazo katika hoja nani hasa anayehusika na maisha ya kijamii anayepaswa kuhakikisha
uwepo wa kanuni na masharti kwa ajili ya mazungumzo: jibu sahihi ni jamii yenyewe,
kukanusha tabia za kuonea wengine au kudharau wengine, kuondokana na ufahari wa kuona
dini yangu ni bora kuliko ya yule, vivyo hivyo haki za waaamini. Huu ni mlango kwa
ajili ya kuingia katika mazungumzo na mtu wa dini nyingine.