Wakristo: dumuni katika kuwa ladha ya chumvi ya dunia- Papa
(Vatican Radio) Baba Mtakatifu Francisco, siku ya Jumapili alitoa wito kwa waumini
na watu wote wenye mapenzi mema kudumu katika kuwa ladha ya chumvi ya dunia, katika
huduma mbalimbali, ikiwemo utetezi na utunzaji wa viumbe. Papa alitoa wito huo, akiangalisha
katika adhimisho la Siku ya Maaskofu wa Italia, kwa ajili ya Ulinzi na utetezi wa
viumbe, ambayo Maaskofu wamechagua mwaka huu, kuzingatia kuelimisha katika huduma
kwa ajili ya viumbe. Ni matumaini ya Papa Francisko kwamba kila mtu, kila taasisi,
vyama na wananchi - wataimarisha juhudi zao, ili kulinda maisha na afya ya watu na
Kuheshimu mazingira na asili.
Papa Francisko alitoa wito huo, baada ya hotuba
yake iliyofuatiwa na sala ya Malaika wa Bwana, aliyosali pamoja na mahujaji na mahujaji
na watalii waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa kanisa Kuu ya la Mtakatifu Petro
Vatican.
Kabla ya sala Malaika wa Bwana, Papa alihutubia juu ya somo la Injili
, wakati Yesu alipowaeleza wanafunzi wake juu ya mateso yake, kifo na ufufuo (Mt.
16: 21-27). Papa aliutaja wakati huo kwamba ulikuwa ni wakati muhimu wenye kuonyesha
tofauti dhahiri kati ya njia ya Yesu ya kufikiri na ile ya wanafunzi wake , na hasa
katika tabia ya Petro. Petro, kiongozi wa mitume kumi na wawili kwa fikira zake za
kibinadamu, anamfokea Bwana wake, kwamba hayo hayawezi kumtokea. Papa Francis aliendelea
kufafanua, Yesu, kwa upande wake, pia anamkemea Petro , kwa sababu hakufikiri kwa
mujibu wa Kazi ya Mungu, ila kwa fikira za utendaji wa kibinadamu, na bila ya kutambua
kama ni majaribu na kishawishi cha shetani.
Baba Mtakatifu alisema, Mtakatifu
Paulo kwa somo hili, anatuambia sisi katika barua yake kwa Wakristo wa Roma, tusitende
kwa mitindo ya ulimwengu huu, lakini kwa kufanya upya akili zetu ili tupate kuushinda
mtihani wa maisha kwa kutenda yaliyo mema ya kumpendeza Bwana , na kwa mapenzi kamili
ya Mungu (Rum 12:. 2).
"Kwa kweli, aliendelea Papa Francisko, sisi Wakristo
tunaishi katika ulimwengu huu tukiwa tumechanganyikana kijamii na kiutamaduni kadri
ya hali halisi za wakati wetu, hiyo ni sawa, lakini hii Papa alionya, linaleta hatari
ya kutaka kutenda 'kidunia'. Tutapoteza ladha ya 'chumvi ya Ukristo tusipokuwa waangalifu
'(cf. Mt 5:13). Papa aliwataka Wakristo kuwa macho na maamuzi yanayotolewa kwa fikira
za kunufaisha kidunia tu, mawazo yasiyo mtanguliza Mungu. Alisisitiza kwamba, Wakristo
wanapaswa kuwa kinyume na fikira zote potofu, kama Injili inavyofundisha. Na kwamba
, nguvu ya Injili bado ni hai ndani ya Wakristo, na ina uwezo wa kubadilisha
vigezo vya hukumu za wanadamu, kutathimini maadili, faida zake, na mwelekeo wa mawazo,
vyanzo vya msukumo wake na mifano ya maisha yaliyo tofauti na Neno la Mungu na mpango
wa wokovu.
Mwisho, Papa kwa upendo Mkuu aliwasalimia wote waliokuwa wakimsikiliza,
aliwataja washiriki wa mkutano wa kimataifa wa 5 wa Watunga sheria Katoliki , mkutano
uliofunguliwa huko wiki iliyopita Frascati, nje Roma. Aliwahimiza, waishi kwa moyo
mkuu jukumu lao nyeti la kuwa watetezi wa watu, kulingana na maadili Injili.