2014-09-01 15:46:26

Tunzeni Mazingira kwa ajili ya afya ya watu na miji


Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia katika Maadhimisho ya Siku ya Tisa ya kutunza mazingira, ambayo inaadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe Moja Septemba , mwaka huu inaongozwa na kauli mbiu isemayo kwamba ,kuelimisha kutunza kwaajili ya viumbe, kwa ajili ya afya ya nchi yetu na miji yetu.
Katika ujumbe uliotolewa na Baraza la Maaskofu katoliki Italia unasema kwamba hii ni sauti ya kuunga mkono kwa wale wote wanao lia kwa uchungu sana , kwa sababu ya maafa mengi yaliyojitokeza ya tabia nchi, ya ukame, na ya magonjwa ya kansa yanayotokana na uchafuzi wa hali ya hewa na mazingira.
Ni wito kwa watu wote hili waweze kueneza neno ambalo liwaangazie watukwa ya maisha , na pia neno hili lipate kuwekwa katika matendo kwa kutibu kwa upendo na kuhudumia wale wote wanadamu walio pata majeraha na pia mazingira
Baraza la Maskofu Katoliki Italia wakitumia neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Hosea ( 4,2-3)
“Hapana neno ila kuapa kwa uongo , na kuvunja ahadi, na kuua, na kuiba, na kuzini ; hurka mpaka, na damu hugusana na damu.Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na kila mtu akkaye ndani yake atadhoofika, pamoja na wanyama wa kondeni , na ndege wa angani; naam , samakai wa baharini pia wataondelewa”
Wanasema kwamba utafikiri neno Hosea ameandikwa kwajili ya nyakati zetu hizi , sura hii; kwani inakusanya machungu na mateso , na mahahangaiko ya watu walio wengi wanaoishi katika sehemu zilizochafuliwa nchini Italia na ulimwengu kwa ujumla.
Kutojali muungano kati ya maumbile ya dunia matokeo yake ni uhadui unosababisha umwagaji wa damu , na mioyo ya wengi kujifunga ndani na uoga kwa kila mmoja , kwa sababu yavurugu zinazotokeza na machafuko.
Inabidi kujibidisha kwaajili ya kutunza mazingira ambayo yanahitaji pia kuyapenda , tuyalinda na tuwe na utambuzi wa kweli. Dunia hii ndimo tunamoishi, na wote tunaitwa kwa kazi hiyo ambayo inapaswa pia kuhimizwa mashuleni, hili nao watoto wapate kuwa na mwamko wa utunzaji bora wa mazingira na kati ya vijana.

Utunzaji wa mazingira ni muhimu kwasababu ya kiuchumi na kuzalisha nafas iza kazi, japo inabidi kutokuvuka mipaka ya nchi , bali kuhamasisha kama utajiri, na na uzalishaji na kukua kwa jamiii.
Vijana ni walinzi wa asubuhi na matarajio ni kwao, tunawategemea tena katika nafasi zenye kuwa na furaha, maisha mazuri na baraka; maana neno tena kutoka kwa Hosea linasema: “Nami nitapanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe; nami nitamrehemu yeyé asiyependa rehema; nami nitawaambia wale wasiokuwa watu wangu, ninyi ndinyi watu wangu,nao watasema wewe ndiwe Mungu wangu”
Maadhimisho ya siku hiyo yame unganisha taasisi mbalimbali na mashirika nchini Italia kwaajili ya kuunga mkono juu ya utunzaji wa mazingira.
TANZANIA : Siku ya Ndege Wanaohama Duniani…
Katika kijiji kimoja cha Ramsar karibu na Ziwa Natron wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha , Kuna ndege wazuri wa kuhama waitwao Lesser Flamingo ambao wanavutia sehemu kubwa ya watalii.
Ni eneo karibu km za mraba 2200 kaskazini magharibi mwa Arusha ambapo pamezungukwa na majani mazuri amabpo panajionyesha kundi kubwa la kupendeza la ndege hao Leeser Flamingos.
Katika kuienzi tukio la mwaka huu 2014 la Siku ya Ndege Wanaohama Duniani, Manager wa Ziwa la Natron Bwana Bw. Mihindi Baso wamekaribisha na pia kijiji kizima cha Ngaresero kwa wiki hii kufanya pamoja kumbukumbu ya siku ya ndege wanao hama yenye kuwa na Kauli mbiu “Njia za ya ndege : Kuhama kwa Ndege na Utalii” (Destination Flyways:
Tukio hili limeandaliwa kampeni kubwa inayohusu Maisha ya ndege ya Kimataifa, ni chombo kikubwa cha kimataifa kinachohusika na uangalizi wa viumbe, mazingira ya ndege na wanyama , chombo hiki kinafanya kazi na washiriki 120 za duniani kote .
Tunajua wazi Ziwa Natron kwa Tanzania ni muhimu sana na ya kuvutia, kwa ukubwa na maji yake na wanyama wake .
Kutokana na umuhimu waziwa hilo hata mwakilishi wa Maisha ya ndege kimataifa kutoka nchini Kenya Bwana Kenny Mwathe siku hiyo alisema kuwa Natron ni sehemu ya kuvutia kwa ndege hao Flamingo kwasababu maji yake ya kiasi yanawezesha ndege hao kuishi, kiasi kwamba ndege hao hawaangaiki kwenda pembeni zaidi ambapo wanaweza kukutana na maadui zake.
Nia ya siku hiyo ni nini? Taarifa zilizoandaliwa na shirika la kimataifa la utalii linasema kuwa :
Siku ya Ndege Wanaohama Duniani (WMBD) 2014 inaonyesha uhusiano kati ya hifadhi ya ndege wanaohama, maendeleo ya jamii na utalii kote duniani. Kila mwaka, zaidi ya watalii bilioni moja huvuka mipaka ya kimataifa.
Kama vile wanyamapori ni rasilmali yenye thamani ya nchi pia kuhama kwa wa ndege inayosisimua ni ya thamani kubwa katika sekta ya utalii. Shughuli za kitalii zinazohusika na ndege wanaohama (kwa mfano kuwatazama au kuwapiga ndege picha) zikisimamiwa vizuri zinaweza kuwa msingi thabiti wa kuleta faida katika uhusiano baina ya watu na ndege wanaohama.
Katika kampeini ya mwaka 2014, WMBD ikishirikiana na UNWTO (Shirika la Kimataifa la Utalii) imetilia mkazo njia ambazo ndege wanaohama hufuata katika misimu: yaani ‘Maeneo ndege hupitia wakihama’. Ikiongozwa na Shirika la Kimataifa la Utalii (UNWTO) pamoja na mashirika mengine yenye ujuzi na utaalamu katika nyanja za utalii na hifadhi ya mazingira, ‘Maeneo ndege hupitia wakihama’inayo nia ya kukuza utalii unaostawi katika maeneo ambayo ndege hao hutua wakati wa safari zao (‘Flyways’).
Kwa kutumia mapato kutoka utalii, mpango huu unataka kuyalinda makao ambayo ndege hawa hutua katika safari zao, wakati huo huo ukiwapa wakaazi wa maeneo hayo ajira zinazohusiana na hifadhi ya mazingira. Katika kampeini ya mwaka huu wa 2014, yenye kauli mbiu ‘Maeneo ndege hupitia wakihama’ iwe mfano maalum ya jinsi utalii inayohusika na ndege wanaohama kuweza kuwa chombo cha utunzaji wa mazingira na ustawi wa jamii kwa kuleta faida kwa wanyamapori, wakaazi wa maeneo hayo na pia watalii.
Kwa kauli maana hiyo watu wote waliodhuria siku hiyo waliombwa kuhusika katika kutnza mazingira ya ziwa hilo kwa ajili ya viumbe hivyo.








All the contents on this site are copyrighted ©.