2014-08-30 11:21:13

Mawaziri wa Afya Afrrika Magharibi wajadili mikakati ya kupambana na ebola


Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola, safari za ndege kuelekea Afrika Magharibi zilikuwa zimepigwa marufu.Mawaziri wa Afya kutoka nchi za Afrika Magharibi, wamekubaliana kuondoa upigaji marufu huo wa safari za ndege, na ufungaji wa mipaka kwa nchi zilizoathirika kutokana na ugonjwa wa Ebola.
Mawaziri hao ambao wamekutana mjini Accra, Ghana kupitia na kuangalia kwa upya mikakati iliyokuwa ikitumika kupambana na virusi vya ebola na pia wametoa ombi maalum kwa mashirika ya ndege kurejesha safari zao katika nchi zilizoathirika.

Mawaziri wa afya wamesisitiza mkakati wa pamoja kuwa bado ni mpango bora kabisa katika kupambana na ugonjwa wa ebola. Mawaziri hao wamezitaka nchi kutofunga mipaka yao kwa nchi zilizoathirika lakini wabakie kuwa waangalifu.

Pia wamekubaliana kuongeza raslimali kwa watu ikiwa ni pamoja na kutakiwa wafanyakazi wa afya kwa haraka , vifaa vya kujikinga na ugonjwa huo, na vituo vya kuwahifadhi wagonjwa.

Shirika la Afya la Afrika Magharibi lina wiki moja ya kuandaa hatua za kuchukua na kuandaa bajeti ili kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani na wadau wengine.

Waliodhuria mkutano huo ni Mawaziri wote wa afya wa kutoka nchi zilizoathirika kutokana na ugonjwa wa ebola za Guinea, Sierra Leone, Liberia na Nigeria, wengine waliobaki hawakuweza kuhudhuria kutokana na matatizo ya ndani na matatizo ya usafiri wa ndege ambao umesitishwa katika nchi zilizoathirika.
Mawaziri wa afya wametoa ombi maalum kwa mashirika ya ndege kurejesha safari za ndege na kuendelea kuruka kwenda katika nchi zilizoathirika.
Hata hivyo wamesisitiza upimaji wa joto la mwili na kuhakikisha usafi wa mikono katika vituo vya kuingia na kutoka.


SHIRIKA LA AFYA DUNIANI WHO
Pamoja na harakati hizo zinazofanyika, bado kuna ofu ya kuambukizwa watu 20,000 na Ebola, kama shirika la afya WHO duniani linavyoripoti huko Afrika Magharibi.
Shirika hilo la Afya limeonya kuwa mlipuko huo huenda ukasambaa na kambukiza zaidi kabla haujadhibitiwa.

Kwa sasa idadi ya waliothibitishwa na kuorodheshwa kuambukizwa ni elfu 3 ingawaje inashukiwa kuna watu wengi ambao hawajajulikana.
Hadi sasa zaidi ya watu 1500 wamefariki kutokana na mlipuko wa sasa wa Ebola wengi wao wakiwa ni wa kutoka nchi za Liberia,Sierra Leone na Guinea.
Mkurugenzi wa (WHO) katika kanda hiyo - Dr Lious Sambo - ameeelezea jinsi wafanyakazi katika kliniki za wagonjwa wanavyoanagaika sana wakijaribu kukabilianana na janga hilo la Ebola.
Wauguzi ni wachache na kwa wakati huo wanapaswa kusaidia haraka inavyowezekana.

TUZIJUE NJIA TANO ZA KUJIEPUSHA VIRUSI VYA EBOLA NA DALILI ZAKE.

Ebola ni mojawapo ya virusi hatari zaidi ulimwenguni lakini haiambukizwi kupitia hewa, hivyo basi huwezi kuambukizwa Ebola kama homa ya kawaida.
TUZIJUE NJIA TANO ZA KUJIEPUSHA VIRUSI VYA EBOLA NA DALILI ZAKE.

Ebola ni mojawapo ya virusi hatari zaidi ulimwenguni lakini haiambukizwi kupitia hewa, hivyo basi huwezi kuambukizwa Ebola kama homa ya kawaida.
Madaktari wanasema kuepuka Ebola ni rahisi sana iwapo mtu atafuata tahadhari hizi muhimu zaidi: Njia ya kwanza ni sabuni na maji. Nawa mikono kila baada ya shughuli yeyote kwa kutumia sabuni na maji safi- na utumie taulo kujikausha.
Hili huwa jambo gumu kwa wanaoishi kwenye makazi duni, na walio vijijini ambako aghalabu maji safi hayapatikani moja kwa moja- lakini ni mbinu iliyothibitishwa ya kuua virusi vya Ebola.Unachohitaji tu ni sabuni ya kawaida.


Kusalimiana kwa mikono kunafaa kuepukwa kwa ujumla, daktari Unnis Krishnan wa Plan International aliarifu BBC, kwamba Ebola husambazwa haraka watu wanapowasiliana ana kwa ana na maji maji ya kimwili ya waliougua.Na dalili ya ugonjwa huu huchukuwa muda kabla ya kudhihirika, hivyo inabidi kutumia njia zingine za kujuliana hali.

Njia ya pili ni hakuna kugusana:Iwapo unashuku kuwa mtu ana Ebola, usimguse.
Inaokena kuwa si maadili mema unapoona unaowapenda wakihisi uchungu na unataka kuwakumbatia na kuwahudumia, lakini maji maji ya kimwili- mkojo na kinyesi, matapishi, kamasi, mate, machozi, na mbegu za kiume na majimaji ya uke- vyote huweza kueneza Ebola.


Dalili za mtu aliyeugua ni joto mwilini, maumivu kwa misuli na viungo, vidonda kooni, kuumwa na kichwa, na uchovu- kufuatiwa na kichefuchefu, kutapika, na kuharisha, ambapo mtu huweza kutoa damu pia. Watie watu hao moyo kutembelea kituo cha afya haraka iwezekanavyo.

Pia ni uamuzi mzuri usiguse nguo au vifaa anavyolalia hao waliougua Ebola- kwani na Medecins Sans Frontieres anashauri kuwa malazi ya waliougua yanafaa kuteketezwa.

Njia ya tatu ni kuepuka miili ya wafu:
Iwapo unadhani mtu amefariki baada ya kuugua Ebola, usiguse mwili wao, hata kama ni mila au desturi ya maziko. Baada ya mtu kufa, bado unaweza kuambukizwa Ebola kutoka kwa miili yao kwani bado inatoa maji maji ya mwili ambayo huweza kuwa hatari zaidi hata kuliko ya mtu alieugua. Fanya mipango kupata timu ya walioandaliwa kushughulikia mwili huo haraka iwezekanavyo kwani ni hatari kuwacha mwili wa mfu kwa muda mrefu katika eneo la makazi.

Njia ya 4. Usile nyama ya porini
Epuka kuwinda, kugusa, au kula nyama ya porini, kwa mfano popo, nyani na sokwe, kwani wanasayansi wanaamini kuwa hiyo ndiyo chanzo cha maambukizi kwa binadamu. Hata kama mnyama fulani wa porini huliwa katika eneo lenu na nyama yake ni tamu epuka myama huyo kwani nyama yake au damu yake huweza kuwa na virusi hivyo. Na hakikisha vyakula vyote vinapikwa inavyostahili.

Njia ya 5. Usiwe na hofu
Kueneza uvumi huongeza hofu. Usiogope wafanyakazi wa huduma za afya- wako hapo kukusaidia na kliniki ndipo mahali mwafaka kwa mtu kuponywa- wataongezewa maji na kutulizwa maumivu.
Takriban nusu ya watu walioambukizwa Ebola kufuatia mzuko wa hivi punde wa Ebola walifariki.

Kumekuwepo na matukio ya madaktari kushambuliwa na watu kutorokwa wanaposhukiwa kuwa na Ebola- hata wakati wanaugua ugonjwa tofauti.
Kuamini matibabu ya kiasili ambayo hayajathibitishwa kutoa afueni, pia kumechangia ongezeko la kuenea kwa virusi vya Ebola.

"Kinga ndiyo njia bora zaidi ya kukabiliana na Ebola, hivyo basi epuka na kuacha uvumi na usiwe na hofu; inawezekana kupunguza maumivu na kuokoa maisha,” daktari Krishnan alisema ugonjwa wa virusi vya Ebola (EVD) unazo dalilii zake amabazo ni homa, kuvuja damu na kuharibika kwa mfumo mkuu wa neva.
Maafa ya ugonjwa huu huweza kufikia hadi asilimia tisini- lakini mzuko wa hivi punde unasababisha maafa ya 55% .

Ugonjwa huo huchukua muda wa siku ishirini na moja kukomaa.
Hakuna kinga wala tiba, bali huduma za msaada na kudhibiti kupoteza maji mwilini kutokana na kuharisha au kutapika husaidia katika kuponaInafikiriwa kuwa popo ndo vilemea vya ugonjwa huo.








All the contents on this site are copyrighted ©.