Papa atuma rambirambi kwa kifo cha Albert Reynolds
Kufuatia kifo cha Taoiseach Albert Reynolds aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ireland, aliye
fariki Agosti 21, 2014, Baba Mtakatifu Francisko, alipeleka salaam zake za rambirambi
kwa Mke wa Marehemu Reynolds, watoto wake na familia yake. Hati ya rambirambi za
Papa, ilitiwa sahihi na Katibu wa Jimbo la Papa, Kardinali Pietro Parolin. Salaam
hizo zilizomwa hadharani siku ya Jumatatu wakati wa mazishi ya Marehemu Taoiseach
Alibert, baada ya Ibada ya Misa na Maziko iliyoongozwa na Askofu Mkuu Diarmuid Martin,
wa Jimbo Kuu la Dublin, katika Kanisa la Moyo Mtakatifu la Donnybrook, Dublin.
Katika
rambirambi hizo, Papa alionyesha ukaribu wake kwa familia Reynolds na kutoa baraka
zake za kichungaji pia kwa wote waliohudhuria mazishi hayo.
Reynolds, ambaye
amefariki akiwa na umri wa miaka 81, anakumbukwa kwa kazi kubwa aliyoifanya wakati
wa mchakato wa kutafuta amani Ireland ya Kaskazini, na wakati wa utawala wa kihistoria
wa kijeshi ya Ireland, na kusitishwa kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1994.
Alikuwa Waziri Mkuu tangu Februari 1992 hadi Desemba 1994.