Jumatano, Baba Mtakatifu Francisko, alikutana na Dr Paul Bhatti, Waziri wa zamani
kwa ajili ya Mshikamano wa Kitaifa na makundi madogomadogo ya waumini wa dini mbalimbali
Pakistani. Dk Bhatti alikuwa kati ya waliohudhuria Katekesi ya Papa ya Jumatano,
akiwa yeye na mama yake, wote wawili ni wakatoliki.
Dr Bhutti ambaye ni ndugu
wa Shabhz Bhatti , aliyeuawa kikatili mwaka 2011 na mashabiki wa Uislamu, alipata
muda mfupi wa kuzungumza na Papa Franciko. Baba Mtaktifu Francisco katika maongezi
yao alionyesha masikitiko yake kwamba Wakristo wengi wanaendelea kuteseka duniani
kote kutokana na imani yao. Nae Dr Bhatti na mama yake walitoa mwaliko kwa Papa Francisco
, aitembelee jumuiya ndogo Wakristo Pakistani.
Dr Bhutti baada ya kukutana
na Papa aliwaambia wanahabari kwamba, kwake imekuwa ni heshima kubwa na muda muhimu
na wa kipekee. Na katika mahojiano na Redio Vatican, aliikosoa jumuiya ya kimataifa
kwamba, kuna udhaifu katika utendaji wake hasa katika kukomesha mateso na mauaji
dhidi ya Wakristo. Na kwamba ni muhimu kutambua mzizi wa ubabe wa kidini na ughaidi
na kuupatia dawa ya kukomesha. Aidha alizungumzia ujasiri wa baadhi ya Waislamu wasiokuwa
na ubabe wanaotetea Wakristo na kulaani vikali unyanyasaji wa watoto, na hasa utiaji
wa kasumba tangu wakiwa na umri wa mdogo kutoogopa kuua.