2014-08-28 16:23:45

Kanisa Katoliki Zambia lajiunga katika kupambana na ugonjwa wa ebola


Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia, kwa pamoja na Mashiriika kadhaa ya kujitegemea NGOs, wamepata vipeperushi vyenye maelezo juu ya virusi vya ebola, vilivyoandaliwa kwa ajili ya zambia na na Shirika la Misaada Katoliki Caritas (CRS). Mwakilishi wa CRS Zambia Dane Fredenburg, akitoa maelezo juu ya vipeperushi hivyo alisema, shirika lke liko makini katika kuhakikisha kwamba jamii inapata ufahamu wa kutosha juu ya ugonjwa wa ebola . Na kwamba CRS, ina hamu ya kutoa habari zaidi za hakika juu ya ugonjwa huo kwa ajili ya kuhamsisha pia mashirika mengine na Makanisa katika utoaji wa habari hizi muhimu kwa ajili ya afya ya umma, na hasa katika ngazi ya vituo vya afya vijijini.

Na kwamba, makanisa yanalengwa zaidi kutokana na ukweli kwamba, Kanisa Katoliki hutoa karibu 70% ya huduma za afya vijijini nchini Zambia, na hivyo kuliwezesha Kanisa kuwa na vifaa vya habari, kwa ajili ya kufanikisha utoaji wa habari hizi kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na utundikaji wa mabango , vipeperushi na vyombo vingine vyamawasiliano jamii kama redio na magazeti, katika Jitihada za kupambana na habari potofu zinazotolewa na baadhi ya watu juu ya ugonjwa wa rebola na kuleta hofu kubwa kwa jamii.

Zambia, mwezi huu, ilipiga marufuku watu kuingia nchini humo kutoka nchi za Afrika Magharibi ambapo ugonjwa wa Ebola umezuka. Hata hivyo, Waziri wa Afya nchini Zambia, Joseph Kasonde amekanusha uwepo wa rufuku hiyo katika kusafiri akisema kwamba, kauli iliyotolewa ilikuwa inashauri watu kwa watu huu kuahirisha mipango ya kwenda katika nchi zenye kuwa na wagonjwa wa ebola. Na kwamba, ushauri huo ni tahadhari tu ya kuhakikisha virus vya Ebola haviingia Zambia. Aidha Serikali ya Zambia imetangaza kuweka katiak milango ya mipaka yake yote ukaguzi wa afya kwa watu wote wanaoingia Zambia.
Aidha taarifa inabaini,mwishoni mwa wiki, Serikali ya Afrika Kusini pia ilitoa tamko la dharura lililopiga marufuku kwa wasiokuwa raia wa Afrika Kusini kuingia nchini huko kutoka katika nchi zilizoathirika na ugonjwa wa ebola. Waziri wa Afya Aaron Motsoaledi alinukuliwa na Shirika la Utangazaji Afrika Kusini kuweka jumla ya kupiga marufuku kusafiri kwa ajili ya wote wasiokuwa raia kusafiri kutoka nchi tatu za Guinea, Liberia na Sierra Leone. Na raia wa Afrika Kusini wenye kuwa na mipango ya kwenda katika nchi zilizoathirika na ebola wameombwea kuahirisha mipango yao kwa wakti huu. Pia Kenya imetoa tamko kama hilo.

Hata hivyo , Shirika la Afya Duniani, linakatisha tamaa mashirika ya ndege na nchi zinazotaka kupiga marufuku watu kufany asasafi katikanchi athirika, ili kuepuka kwa nchi hizo tatu za Afrika Magharibi, kutenga na dunia. Linachosisitiza zaidi, ni watu kupata melezo sahihi ya ugonjwa huu hasa dalili zake ili kwamba mara tu wanapiohisi kuwa na za Ebola kufika hospitalini mara moja na ugonjwa huu humwingia mtuu mwingine kwa kushika majimaji kuoka kwa mwenye kuwa na virus.








All the contents on this site are copyrighted ©.