Yapita miaka hamisini ya mauaji ya Mwenye Heri Marie-Clementine Anuarite Nengapeta
Katika tukio la kuadhimisha kutimia miaka 50, tangu Mwenye Heri Marie Clementine Anuarite
Negapeta kukabiliwa na kifo dini, Kanisa Katoliki Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
litafanya kilele cha maadhimisho ya jubilee hii katika Makazi Shirika la Familia
Takatifu, Kisangani.
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu, Padre Leonard Santedi,
Jumatano wiki hii, aliwasilisha kwa waandishi wa habari, ratiba ya jubilee hii ,
kwamba, kwanza kutakuwa na mipango mfululizo ya kuongeza uelewa zaidi juu ya maisha
ya Sista Nengapeta kwa ajili ya kukuza moyo wa ibada, pili, itakuwa ni hija ya kitaifa
katika madhabahu ya Isiro na Wamba na tatu ni kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya
ujenzi wa Kanisa Kuu la Isiro, ambalo ilitapewa heshima ya Mashahidi wafia dini.