Cheche za makubaliano ya amani zaanja kujionesha Msumbiji
Serikali ya Msumbiji na Chama cha upinzani cha RENAMO zimetiliana sahihi mkataba wa
amani na hivyo kung'oa mzizi wa fitina ulioibuka kwa kasi kubwa katika kipindi cha
miezi kadhaa iliyopita kiasi cha kuzua hofu ya kuzuka tena kwa vita ya wenyewe kwa
wenyewe nchini Msumbiji.
Makubaliano haya yamefikiwa baada ya majadiliano
ya muda mrefu kati ya Serikali na RENAMO na hivyo kuanza kuweka mikakati ya uchaguzi
mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo tarehe 5 Oktoba 2014. Pande hizi mbili zinaendelea
kujadiliana namna ya kutekeleza makubaliano ya pande hizi mbili. Chama cha upinzani
cha RENAMO kimemteuwa Alfondo Dhlakama kupeperusha bendera ya chama hiki wakati wa
kinyang'anyiro cha Urais nchini Msumbiji.