2014-07-30 08:58:26

Tovuti kwa ajili ya hija ya kitume ya Papa Francisko Korea ya Kusini


Baraza la Maaskofu Katoliki Korea hivi karibuni limezindua tovuti maalum kwa ajili ya kuwasaidia waamini na watu wenye mapenzi mema wanaotaka kufuatilia kwa karibu zaidi hija ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Korea, itakayoanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 14 hadi 18 Agosti 2014. 00:01:54:84

Hii ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Sita ya Vijana Barani Ulaya inayoongozwa na kauli mbiu “Ondoka, uangaze, kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Bwana umekuzukia”, maadhimisho ambayo yatafanyika Jimboni Daejeon, Korea ya Kusini. Kwa wale wanaopenda kufuatilia matukio haya wanaweza kutembelea katika tovuti ifuatayo:

Tovuti hii inapatikana kwa lugha ya Kiingereza na Kikorea. Mtandao huu una utajiri mkubwa wa habari, matukio yatakayokuwepo, liturujia, sala na maana ya tukio hili la kihistoria. Nembo inayoongoza hija hii ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko inachota utajiri wake kutoka katika maneno ya Nabii Isya, “Ondoka, Uangaze”.

Nembo inaonesha mtumbwi na miale ya moto inayoiangazia dunia, changamoto kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema Barani Asia na Korea kwa namna ya pekee kutembea katika mwanga wa Bwana. Itakumbukwa kwamba, Baba Mtakatifu pia anatarajiwa kuwatangaza Watumishi wa Mungu 124 kuwa Wenyeheri. Ibada ya Misa Takatifu kwa aliji ya kuwatangaza Mashahidi hawa kutoka Korea, inatarajiwa kuadhimishwa hapo tarehe 16 Agosti, kwenye mji wa Guanhwamoon.

Baba Mtakatifu Francisko anafanya hija hii ya kitume nchini Korea, ikiwa imekwisha kutimia miaka 25 tangu Mtakatifu Yohane Paulo II alipotembelea Korea kunako mwaka 1989, ili kushiriki katika Maadhimisho ya Kongamano la Ekaristi Takatifu Kimataifa.








All the contents on this site are copyrighted ©.