2014-07-18 09:56:20

RAI na CTV kushirikiana kwa karibu zaidi!


Kituo cha Televisheni cha Vatican, CTV, tarehe 17 Julai 2014 kimetiliana sahihi mkataba wa ushirikiano na Kituo cha Televisheni cha Taifa la Italia, RAI, ili kusambaza kwa kina na mapana matukio mbali mbali yanayotekelezwa na Baba Mtakatifu Francisko katika maisha na utume wa Kanisa. Tukio hili limehudhuriwa na Askofu mkuu Angelo Becciu, Katibu mkuu msaidizi wa Vatican pamoja na wakuu na wafanyakazi wa mtandao wa Rai, kwenye makao makuu ya RAI yaliyoko mjini Roma.

Mkataba huu umewekwa sahihi na Bwana Luigi Gubitosi, Mkurugenzi mkuu wa RAI pamoja na Monsinyo Dario Edoardo ViganĂ², Mkurugenzi mkuu wa Kituo cha Televisheni cha Vatican. Makubaliano haya yanapania kuimarisha ushirikiano kati ya huduma inayotolewa na RAI pamoja na Vatican. RAI pia itashiriki katika kurusha matangazo wakati wa Katekesi za Baba Mtakatifu, Ibada na maadhimisho mbali mbali yatakayofanywa na Baba Mtakatifu ndani ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro au kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.