2014-04-23 15:00:29

Mshikamano wa dhati kutoka kwa Papa Francisko kwa wafanyakazi wanaohofia hatima ya maisha yao!


Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya Katekesi yake, Jumatano, tarehe 23 Aprili 2014 ameonesha masikitiko na mshikamano wake wa dhati kwa wafanyakazi wa kiwanda cha kufua chuma, kilichoko Piombini, Kaskazini mwa Italia, waliomwomba kuwatembelea kabla kiwanda hiki hakijafungwa.

Baba Mtakatifu anasema, nyuso za wafanyakazi hawa zilionesha masikitiko makubwa na wasi wasi kuhusu hatima ya maisha ya familia zao. Wafanyakazi hawa anasema Baba Mtakatifu wanachoomba ni haki ya kufanya kazi, ili waweze kuishi kwa heshima, ili kuwatunza, kuwalisha na kuwaelimisha watoto wao. Baba Mtakatifu amewahakikishia uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala na kamwe wasikate tamaa, ili kuamsha tena moyo wa matumaini yanayobubujika kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambayo kamwe hayawezi kudanganya.

Baba Mtakatifu anawaomba viongozi wanaohusika kujitahidi kuhakikisha kwamba, wanatekeleza wajibu wao kwa kuzingatia kipaji cha ugunduzi na ukarimu, ili kuwawashia tena matumaini wafanyakazi ambao wamekata tamaa kutokana na madhara ya mtikisiko wa uchumi kimataifa, ambao umesababishwa na baadhi ya watu kutoguswa na mahangaiko ya jirani zao.







All the contents on this site are copyrighted ©.