2014-04-22 10:42:09

Pasaka ni kielelezo cha hali ya juu cha upendo wa Mungu kwa binadamu!


Uhuru wa kweli ni ule unaomkirimia mwanadamu ukombozi kutoka katika lindi la dhambi na mauti. Kutokana na mantiki hii Msalaba wa Kristo umekuwa ni kielelezo cha ukombozi na upatanisho kati ya Mungu na binadamu; mwaliko kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema kujipatanisha wao kwa wao, ili kujenga msingi wa haki, amani, upendo na mshikamano wa kidugu.

Kwa njia ya Fumbo la Pasaka, Mwenyezi Mungu amejipatanisha na binadamu na hivyo kuanzisha Agano Jipya na la Milele. Hii ni sehemu ya ujumbe wa Pasaka kutoka kwa Patriaki Teodori wa Pili wa Kanisa la Kikoptik la Kiorthodox la Alexandria. Anasema, Ufufuko wa Kristo ni tukio muhimu sana katika maisha na utume wa Kanisa.

Msalaba wa Kristo ni kielelezo cha maisha mapya, mwaliko kwa Wakristo kujikita katika majadiliano ya kiekumene, ili kweli umoja miongoni mwa Wakristo uweze kufikiwa kadiri ya matakwa ya Roho Mtakatifu.

Pasaka ikiweza kuadhimishwa siku moja na Makanisa yote, huu utakuwa ni ushuhuda wa imani tendaji na mwanzo mpya wa majadiliano ya kiekumene miongoni mwa Wakristo!







All the contents on this site are copyrighted ©.