Kardinali Roger Etchegaray kutunukiwa tuzo la Msalaba wa heshima!
Bwana Manuel Valls, Waziri mkuu wa Ufaransa, ni kati ya wageni mashuhuri wanaotarajiwa
kuhudhuria katika Ibada ya Misa Takatifu wakati wa kuwatangaza wenyeheri: Yohane wa
XXIII na Yohane Paulo II kuwa watakatifu, hapo tarehe 27 Aprili 2014, kwenye Uwanja
wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Ibada inayotarajiwa kuongozwa na Baba
Mtakatifu Francisko.
Akiwa mjini Roma, Waziri mkuu wa Ufaransa anatarajiwa
kumtuza Kardinali Roger Etchegaray, Rais mstaafu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni
Msalaba wa Heshima, kwa kutambua mchango wake katika kukuza na kuendeleza utamaduni
ndani na nje ya Kanisa. Hii ni heshima ya hali ya juu kutolewa na Serikali ya Ufaransa
kwa watu ambao wamejipambanua kutokana na mchango wao kwa Nchi na Jumuiya ya Kimataifa.