Askofu Konrad Krajewiski wa Vatican, Alhamisi alitembelea na kuwasilisha vitabu
vya Injili, vitabu vidogo zaidi ya 1,000 kwa wafungwa, katika Gereza Kuu la jiji
la Roma ( Regina Coeli). Vitabu hivi vya Injili, vidogo, vinavyo weza kuwekwa mfukoni
, ni zawadi Papa ya Pasaka, iliyoanza kusambazwa tangu Aprili 6, wakati wa sala ya
Malaika wa Bwana katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Askofu Krajewski,
akizungumzia ziara yake katika gereza hilo , amesema ilikuwa ni ya kugusa sana . Wafungwa
wengi walionyesha hisia za kuwa na mapenzi makubwa kwa Papa. Na wengi walieleza matatizo
mengi ya maisha jela , miongoni mwa mambo mengine , ukosefu wa nguo .Na kwamba wafungwa
wa gereza hilo, waliipokea kwa furaha zawadi ya Papa, wakisema kwamba daima watakuwa
karibu na Papa, ingawa wako ndani ya jengo, lililo katika umbali wa kutembea kwa miguu
kufika katika Makazi ya Kalifa wa Mtakatifu Petro . Baadhi ya wameomba , Papa awatembelee,
kwa ajili ya kuwapatia faraja na matumaini katika haki. Askofu Krajewski, ameeleza
na kusema daima ni kuikumbuka neema ya Mungu, na Msamaha wa Yesu Kristo. Wakati wa
kuwasilishwa kwa zawadi hii, pia alikuwepo Kasisi wa Gereza hilo, Padre Vittorio
Trani . Ziara ilichukua muda wa saa moja na nusu .