2014-04-17 08:21:51

UNICEF ina laani vikali kitendo cha utekaji wa watoto wa shule nchini Nigeria!


Shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF linalaani vikali kitendo cha Kikosi cha kigaidi cha Boko Haram kuwateka nyara watoto mia moja na ishirini na tisa wenye umri kati ya miaka kumi na miwili hadi miaka kumi na saba, mapema siku ya Jumatatu, walipokuwa shuleni kwao, mjini Born.

UNICEF inawataka wahusika kuwaachilia mara moja watoto hao ili waweze kuendelea na masomo yao. UNICEF inaendelea pia kulaani mashambulizi yanayofanywa dhidi ya shule nchini Nigeria, kwani Mwezi Februari, 2014, watoto hamsini na tatu wa shule ya msingi waliuwawa kinyama, jambo ambalo haliwezi kukubaliwa na Jumuiya ya Kimataifa kwani ni kinyume cha haki msingi za binadamu pamoja na kuwanyika watoto hao haki ya kupata elimu.

UNICEF inapenda kuonesha mshikamano wake wa dhati kwa wazazi, ndugu na jamaa walioguswa na vitendo hivi vya kigaidi. Ni wajibu wa Serikali ya Nigeria kuhakikisha kwamba, watoto wote waliotekwa wanaokolewa na kurudishwa tena kwa wazazi wao pamoja na kuendelea kupata elimu katika mazingira yenye usalama zaidi.







All the contents on this site are copyrighted ©.