2014-04-17 09:28:24

Kiasi cha dolla za kimarekani millioni 274 zinahitajika ili kuwahudumia wakimbizi


Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa pamoja na Mashirika ya Misaada Kimataifa yanahitaji kiasi cha dolla za kimarekani millioni mia mbili sabini na nne, ili kugharimia operesheni maalum kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi wanaotafuta hifadhi ya maisha. Zaidi ya watu laki mbili wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na vita inayoendelea huko Jamhuri ya Watu wa Afrika ya kati.

Shirika la kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema, idadi ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia wakimbizi laki tatu na sitini na mbili elfu hadi kufikia mwishoni mwa Mwaka 2014. UNHCR inahitaji kiasi cha dolla za kimarekani millioni mia mbili na sabini na nne ili kusaidia operesheni ya kuwahudumia wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi maalum.







All the contents on this site are copyrighted ©.