2014-04-16 07:33:47

Mchango wa Umoja wa Ulaya katika mapambano dhidi ya virusi vya Ebola


Umoja wa Ulaya umeamua kuongeza msaada wake katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola kwa nchi zilizoko Afrika Magharibi kwa kutoa kiasi cha Euro millioni moja. Msaada huu utatumika kwa ajili ya kutoa matibabu pamoja na kupima athari zilizosababishwa na ugonjwa wa Ebola sanjari na kutoa vipimo vitakavyosaidia kuharakisha upimaji wa virusi vya Ebola kwa wagonjwa watakaokuwa wameambukizwa.

Hayo yamebainishwa na Kristalina Georgieva, Kamishina wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia ushirikiano wa kimataifa, ambaye anakazia umuhimu wa kuharakisha mapambano dhidi ya virusi vya Ebola, huko Guinea na nchi jirani ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Ebola.

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kwamba kuna watu 108 waliofariki dunia na wengine 168 wanadhaniwa kwamba, wameambukizwa virusi vya Ebola. Jumuiya ya Kimataifa kwa sasa inaendesha kampeni dhidi ya virusi vya Ebola kwa kushirikiana na Wizara za Afya kutoka katika nchi ambazo zimetikiswa na ugonjwa huu.








All the contents on this site are copyrighted ©.