2014-04-15 10:47:03

Sadaka ya Ijumaa Kuu kwa ajili ya kudumisha uhai wa Kanisa Mashariki ya Kati


(Vatican Radio) Sadaka itakayokusanywa siku ya Ijumaa Kuu katika Parokia zote duniani, kama ulivyo utaratibu wa miaka mingi , itapelekwa kusaidia Makanisa katika Nchi Takatifu. Aidha sehemu ya makusanyo hayo ya sadaka ya Ijumaa Kuu watapewa Wafranciskani wanaojishugulisha na kazi za Ulinzi katika maeneo Matakatifu katika nchi Takatifu .

Wafranciskani walipewa dhamana ya kutunza maeneo Matakatifu tangu mwaka 1209. Licha ya kuwa walinzi pia huwa na miradi ya kusaidia maskini , huendesha shule ,kutoa ufadhili kwa wanafunzi, na kuendesha kazi za kichungaji kwa ajili ya kudumisha uhai wa Ukristu katika nchi hiyo ambako ni asili yake Ukristu .

Kardinali Leonardo Sandri, Mkuu wa Shirika linalo unganisha Makanisa ya Mashariki ya kati, ametoa wito kwa Wakatoliki wote kutoa sadaka yao kwa moyo wa ukarimu zaidi kwa ajili ya kusaidia kudumisha usimamizi wa Usharika wa Makanisa ya Mashariki, kwa kuwa ukusanyaji wa sadaka hiyo, bado hata leo ni chanzo kikuu cha mapato kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kuleta uhai na kazi za Wakristo kanda hiyo.
Kardinali Sandri ameitaja hali ya sasa katika kanda hiyo ,kuwa ni teke, ikiwa imelemewa hasa na machafuko ya vita nchini Syria, mivutano ya kisiasa Misri na kati ya Israel na Palestina .

Na kwamba, Wakristo katika mikoa mbalimbali ya Mashariki ya Kati, wanakabiliwa na changamoto kulihama eneo hili, kutokana na hatari nyingi za kushambuliwa au kuteswa na vurugu na ubaguzi unaofanywa na waislamu wasio vumilia imani zingine. Hata hivyo Wakristu hao wanaendelea kuukiri ukweli wa imani ya Kikristo na hivyo sote katika Kristo tumeunganishwa nao. Na hivyo sadaka inayokusanywa Ijumaa Kuu kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki huwa ni msaada mkubwa kwa Wakristo wa madhehebu mbalimbali kubaki katika kanda kama mashahidi hai kwa Kristo.
Shughuli za kijamii na misaada.
Ili kusaidia Wakristo kubaki katika Nchi Takatifu, ikiwa ni pamoja na wanandoa maskini na vijana, Wafransisko chini ya mpango wa ulinz, wamejenga makazi zaidi ya elfu, katika maeneo mbalimbali - Bethlehemu, Bethfage na Nazareth . Katika Mji Mkongwe wa Yerusalemu kuna 80 nyumba, zilizo fanyiwa Ukarabati za familia za Kikristo . Na pia kimejengwa kituo kikubwa kwa ajili ya huduma Bethlehemu na Nazareth. Pia huduma ya afya hutolewa kwa wahitaji masikini .
Pamoja na hilo kuna pia mipango ya ufadhili wa elimu tangu chekechea hadi Chuo Kikuu. na Wafranciskani hao huendesha shuguli za kichungaji kaitka Parokia 29 ambamo mna miradi ya vijana na familia na vituo vya Parokia mpya katika Jericho na Kana.
Na kuna kituo cha mawasiliano ambaho huelezea historia ya nchi Takatifu katika kwa njia ya tovuto za mawasiliano na kusikika duniani kote katika lugha zaidi ya saba . Pia wanashirika wa ndugu wadogo wa Mtaktifu Francis, huandaa ibada za kiliturujia kwa Wakristo namahuaji ,wakishirikishana na jumuiya zingine za Kikristo katika mfumo wa Kiekumeni.








All the contents on this site are copyrighted ©.