MaskaniRadio Vatican
Radio Vatican   
more languages  
Jumuiya na vyama vya kiroho ni kazi ya Roho Mtakatifu - Papa

Ijumaa hii, Baba Mtakatifu Francisco amekutana na wajumbe kutoka jumuiya Katoliki za udugu na usharika, ambao wako Roma kwa ajili ya Mkutano wao wa Kimataifa wa 16, uliofunguliwa rasmi na Padre Raniero Cantalamesa, Mhubiri maarufu katika makazi ya Papa.
Hotuba ya Papa Francisco kwa wajumbe wa mkutano huo, amewaongoza washiriki wa mkutano kutafakari kwa kina, maana ya kuwa na umoja katika utofauti.

Papa amesema, Umoja haumaanishi usawa; wala haumaanishi kufanya kila kitu pamoja au kufikiri katika njia hiyo hiyo moja. Umoja hauna mana ya mtu kupoteza utambulisho wake. Bali Umoja katika utofauti ni kinyume na hayo, kwa kuwa ni kuitambua furaha ya kujumuika na wengine na kuzikubali tofauti zao mbalimbali kuwa ni zawadi kutoka kwa Roho Mtakatifu, anayo mjalia kila mmoja na ni kuweka ya  ...»Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani (JMJ Rio 2013)
Habari kutoka Vatican 
Sinodi imeliwezesha Kanisa kuona na kusikiliza kwa dhati!

Maadhimisho ya Sinodi maalum ya Maaskofu kwa ajili ya familia ni kielelezo cha mchakato wa Mama Kanisa kutaka kusikiliza kwa dhati kabisa furaha, matatizo na changamoto ambazo familia zinakabiliana nazo katika ulimwengu mamboleo. Ni maneno ya Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu mkuu wa Sinodi za Maaskofu alipokutana na kuzungumza na Wabunge kutoka Uingereza, waliomtembelea mjini Vatican Alhamisi,  ...»


Maisha ya wahamiaji na wakimbizi wengi yako mashakani!

Kardinali Antonio Maria Veglio', Rais wa Baraza la Kipapa la shughuli za kichungaji kwa ajili ya wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum anasikitika kusema kwamba, wahamiaji na wakimbizi wengi watakufa maji pasi na msaada huko baharini kutokana na uamuzi wa Serikali ya Italia kuacha kutoa huduma kwa wakimbizi na wahamiaji waliokuwa hatarini wakati wakijaribu kuvuka bahari kuingia Barani  ...»


Askofu Mbarga ateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Yaoundè, Cameroon

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Jean Mbarga kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Yaoundè, Cameroon. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Mbarga alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki Ebolowa na Msimamizi wa kitume wa Jimbo kuu la Yaoundè.
  ...»Papa ataja wajumbe wapya washauri kwa Shirika la utajaji Watakatifu

Baba Mtakatifu amemteua wajumbe wapya washauri kwa ajili ya Shirika la Utajaji Wenye Heri na Watakatifu. Nao ni Padre Bernard Ardura, O. Praem, Rais wa Kamati ya Kipapa ya Sayansi Historia.; Monsinyori Cifres Alejandro Gimenez, Mkutubu katika Shirika kwa ajili ya Mafundisho ya Imani; Padre Paulo Carlotti, SDB, Mkurugenzi Katika Mahakama ya Kitume ya Kitubio, Padre Tomislav Mrkonjić, O.F.M. .  ...»


Kanisa katika Ulimwengu 
Changamoto za mawasiliano katika ulimwengu wa digitali!

Wakurugenzi wa habari kutoka Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Ulaya kuanzia tarehe 3 hadi tarehe 5 Novemba 2014 watakuwa na mkutano utakaojadili pamoja na mambo mengine mawasiliano kama njia ya kukutanisha watu, kati ya ukweli na utekelezaji wake. Ni mkutano unaolenga kupembua kwa kina na mapana mchango wa Baba Mtakatifu Francisko katika vyombo vya mawasiliano ya kijamii, kama sehemu ya mchakato wa  ...»


Maendeleo ya kweli yazingatie mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili

Jumuiya ya Kimataifa ina wajibu wa kimaadili kulinda na kutetea haki msingi za watu mahalia, lakini kwa kutoa kipaumbele cha kwanza kwa haki msingi za binadamu na uhuru wa kweli, ili kuwashirikisha kikamilifu katika mchakato wa maendeleo yanayozingatia mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili. Sera na mikakati ya maendeleo haina budi kuwahusisha watu mahalia, kwa kuheshimu utambulisho na tamaduni  ...»


Hija ya kichungaji ya Papa Francisko nchini Uturuki, inaonesha matumaini na ujasiri!

Kwa mara ya kwanza Mwenyeheri Paulo VI alitembelea nchini Uturuki kunako mwaka 1967 na Mtakatifu Yohane Paulo II akafanya hija ya kichungaji nchini humo kunako mwaka 1979 na kunako mwaka 2006 Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita akatembelea tena Uturuki.

Kuanzia tarehe 28 hadi tarehe 30 Novemba 2014, Baba Mtakatifu Francisko atafanya hija ya kichungaji inayopania kuimarisha mchakato wa  ...»Habari za Kanisa la Afrika 

Jimbo Katoliki Mahenge tarehe 30 Oktoba 2014 linaadhimisha kilele cha Jubilee ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake kwa kuongozwa na kauli mbiu “Fanyeni yote mapya katika umoja”. RealAudioMP3

Katika maadhimisho haya anasema Askofu Agapiti Ndorobo, mkazo umewekwa kwa wanandoa waliokuwa wanaishi “uchumba sugu” kuhakikisha kwamba, wanarekebisha ndoa zao, mwaliko ambao umeonesha mafanikio makubwa Jimboni ...»


Jimbo Katoliki la Mahenge, Tanzania, linaadhimisha kilele cha Jubilee ya miaka 50 tangu lilipoanzishwa kunako mwaka 1964 na Marehemu Askofu Elias Mchonde aliyekuwa Askofu msaidizi wa Jimbo la Dar es Salaam akateuliwa kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Mahenge na kuliongoza Jimbo hili kuanzia wakati huo hadi mwaka 1969 alipofariki dunia. Baadaye Jimbo limeongozwa na Askofu Nikas Kipengele ...»


Askofu mkuu Paulo Ruzoka wa Jimbo kuu la Tabora, akisaidiana na Askofu mkuu Protase Rugambwa, Katibu mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu ambaye pia ni Rais wa Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa na Askofu mkuu Francisco Padilla, Balozi wa Vatican nchini Tanzania, walikuwa wahusika wakuu katika Ibada ya kumweka Wakfu Askofu Josefu Mlola wa Jimbo Katoliki Kigoma, iBada iliyofanyika ...»


Mpendwa msikilizaji wa kipindi chetu cha Kanisa la nyumbani, Tumsifu Yesu Kristo. Tunakukaribisha kwa mara nyingine tena katika kipindi hiki ambapo kwa uchache tutaangazia yaliyojiri wakati katika wa maadhimisho ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican. RealAudioMP3
Historia yatukumbusha kwamba, Mwenyeheri Papa Paulo VI, ndiye aliyeuendeleza Mtaguso huo na kuzisaini hati zote kumi na sita za mtaguso na zaidi ...»


Askofu Desiderius Rwoma wa Jimbo Katoliki Bukoba ambaye pia ni msimamizi wa kitume wa Jimbo Katoliki Singida, katika mahojiano maalum na Radio Vatican anasema anapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwajalia waamini wa Jimbo Katoliki la Kigoma mchungaji mkuu atakayewaongoza, wafundisha na kuwatakatifuza kadiri ya mapenzi ya Mungu. RealAudioMP3

Anamshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa kumteua Askofu Josefu ...»


Mwaka wa Imani
Muswada wa Katiba Tanzania
Rasimu ya Katiba Tanzania
Hotuba ya Jaji Warioba
Habari za Kijamii na Kisiasa kutoka Afrika 
Afrika inahitaji miaka 60 ili kufutilia mbali baa la umaskini wa kutupwa!

Pengo kati ya matajiri wanaokula na kusaza na maskini, yaani "akina yakhe pangu pakavu tia mchuzi" linaendelea kuongezeka kila kukicha na ikiwa kama ...»


Rais Sata kuzikwa tarehe 11 Novemba 2014

Bwana Roland Msiska Katibu mkuu wa Baraza la Mawaziri Zambia anasema, mwili wa Marehemu Rais Sata unatarajiwa kuwasili nchini Zambia, Jumamosi jioni ...»


Tanzania kujenga maghala makubwa katika mikoa sita na ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kuanza Julai 2015!

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amesema Serikali inalenga kujenga maghala kwenye mikoa sita kupitia mkopo ambao itaupata kutoka Serikali ya ...»


Ben Kiko katangulia mbele ya haki! Atambukwa na wengi enzi zake!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na ...»


Dumisheni utulivu, amani na mshikamano wa kitaifa!

Jukwaa la Wakristo nchini Zambia katika taarifa yake linasema, limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Michael Chilufya Sata, ...»


Habari za Kimataifa kwa ufupi 

Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni alionesha wasi wasi wake kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa wa Ebola sehemu mbali mbali za dunia, lakini kwa namna ya pekee Afrika Magharibi ambako kuna watu wengi wanaendelea kuathirika.

Baba ...»


Taarifa kutoka Umoja wa Mataifa zinaonesha kwamba, kuna kundi kubwa la watoto kutoka Eritrea wanaoingia Barani Ulaya bila ya usimamizi wa wazazi wao, lakini kwa bahati mbaya, hakuna taarifa rasmi zinazoonesha ni watoto wangapi wanaopoteza maisha yao ...»


Bwana Christos Stylianides, Mratibu mkuu wa ugonjwa wa Ebola kutoka Jumuiya ya Ulaya anasema kwamba, kunahitajika jumla ya wataalam 40, 000 mapema iwezekanavyo ili kukabiliana na janga la ugonjwa wa Ebola, huko Afrika Magharibi. Wataalam hawa ...»

Hati za Kanisa 

Baada ya maadhimisho ya Sinodi maalum ya Maaskofu kwa ajili ya familia yaliyoanza hapo tarehe 5 hadi tarehe 19 Oktoba 2014, yakiongozwa na kauli mbiu "Changamoto za kichungaji kuhusu familia mintarafu Uinjilishaji, Mababa wa Sinodi wametoa ujumbe kwa ...»


Mama Kanisa tarehe 19 Oktoba 2014 anaadhimisha Siku ya 88 ya Kimissionari Duniani, iliyoanzishwa kunako mwaka 1926 na Papa Pio wa Kumi na moja na kuanza kuadhimishwa rasmi hapo mwaka 1927 kama siku ya kukoleza ari moyo wa kimissionari katika ...»


Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru Mababa wa Sinodi pamoja na wale wote waliowezesha kufanikisha maadhimisho ya Sinodi maalum ya Maaskofu kwa ajili ya familia. RealAudioMP3

Tukio hili limeonesha umoja na mshikamano katika hija ya pamoja, ambayo wakati ...»


Giovanni Battista Montini, alizaliwa kunako tarehe 26 Septemba 1897 huko Concesio, Brescia, Kaskazini mwa Italia. Baada ya mafunzo na majiundo yake ya kikasisi akapadrishwa kunako tarehe 29 Mei 1920. Baada ya kujiendeleza katika masomo ya Falsafa ...»

TAFAKARI YA NENO LA MUNGU 

Kifo ni kitendawili ambacho binadamu ameshindwa kabisa kukitegua. Anabaki kuhoji na kujihoji bila kupata jibu la kwa nini anakufa. Mbele ya kifo binadamu anabaki kutoa visingizio vya kujitetea na kulaumu, hatimaye anakiona kifo kuwa mwiko. RealAudioMP3

Zamani ...»


Tunakuletea habari njema ya furaha tunapotafakari pamoja Neno la Mungu katika sherehe ya Watakatifu wote. Mama Kanisa akitaka kuhitimisha mwaka wa Kanisa kwa furaha anaona ni vema awaoneshe watoto wake lengo la maisha ya kikristu yaani ni kuelekea ...»


Ijue Radio Vatican Orodha ya vipindi Tafadhali tuandikie kwa anuani ifuatayo Kazi za Radio Vatican Viunganishi kwenye mitandao mingine Lugha nyingine Vatican Jiji la Vatican Maadhimisho ya Liturjia za Kipapa
Haki zote zimehifadhiwa ©. Webmaster / Alama / Masharti ya Kisheria / Matangazo ya biashara